Suala la bondia, Francis Cheka sasa linakwenda mahakamani.
Polisi Morogoro imemtaka mlalamikaji Kaike Siraju ametakiwa kwenda mahamani ili suala lake lifanyiwe kazi huko.
Kaike anamlalamikia Cheka kwa kugoma kupanda katika pambano la ngumi za kulipwa dhidi ya Dulla Mbabe sikukuu ya Krismasi.
Cheka hakutokea kwenye pambano hilo akitaka alipwe fedha zake kwanza huku Kaike akisema alishamtangulizia kiasi fulani na mkataba alisaini.
Polisi Morogoro wameona hakuna sababu ya kumshikilia Cheka na badala yake inaweza kuwa rahisi suala hilo la madai kumalizika mahakamani.







0 COMMENTS:
Post a Comment