December 21, 2016


Kiungo mpya mkabaji wa Simba, Mghana, James Kotei, amefunguka kuwa, kwa mara ya kwanza akicheza Ligi Kuu Bara amekutana na tukio la hatari kutoka kwa wachezaji wa Ndanda FC, lakini anashukuru Mungu amepona.

Kotei ambaye amejiunga na Simba katika dirisha dogo msimu huu akitokea Al Arouba ya Oman, aliitumikia timu yake hiyo mpya katika mchezo wa Jumapili iliyopita dhidi ya Ndanda waliposhinda 2-0, lakini alitoka dakika ya 15 kipindi cha kwanza baada ya kupigwa kiwiko cha mdomo na beki Paul Ngalema.

Mghana huyo amesema kuwa: “Hii ligi ya huku ni ngumu kwa kweli, ushindani niliokutana nao siku ya kwanza si wa kawaida, timu zote zilikuwa kwenye ubora wa hali ya juu.

“Wachezaji wa Ndanda walitaka kunitoa meno, wakati nawania mpira na mchezaji wao mmoja, akanigonga na kiwiko cha mdomo, nikachanika sana mpaka nikashindwa kuendelea na mchezo, japo kwa sasa nipo sawa nafikiri ushindani ni mkubwa sana huku.

Kotei alianza katika mechi hiyo na kuonyesha soka safi lakini alilazimika kwenda nje baada ya kuumizwa.


SOURCE: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic