December 21, 2016



Kiwango cha juu kilichoonyeshwa na beki wa Simba, Abdi Banda katika mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Ndanda FC uliofanyika Jumapili iliyopita kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona, mkoani Mtwara kimemchanganya vilivyo kocha mkuu wa timu hiyo, Mcameroon, Joseph Omog.

Katika mchezo huo ambao Simba ilishinda kwa mabao 2-0, Banda alichezeshwa kama beki wa kati akichukua nafasi Novaty Lufunga, ambaye hivi karibuni amekuwa na matatizo na uongozi wa klabu hiyo.

Omog amesema kuwa hakutegemea kama Banda angeonyesha kiwango kile katika mechi hiyo iliyokuwa na ushindani mkubwa hali inayomfanya ajiulize maswali mengi bila ya kuwa na majibu.

“Hakika Banda alinishangaza sana kwani alionyesha uwezo wa juu katika mchezo huo tofauti na nilivyokuwa nikitegemea, alicheza kwa kujiamini na alikuwa mahiri zaidi katika mpira ya vichwa.


“Kutokana na hali hiyo nitaendelea kumpa nafasi ya kucheza lakini pia kuna kitu kikubwa nimejifunza kutoka kwake,” alisema Omog.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic