December 30, 2016



Kiungo mpya wa Simba, James Kotei, amesema kuwa moja ya vyakula ambavyo vinamfurahisha alivyokutana navyo Bongo ni pamoja na wali na maharage.


Kotei ametua Simba katika usajili wa dirisha dogo akitokea nchini Ghana kwa lengo la kuongeza nguvu katika nafasi hiyo ikiwa ni pamoja na kuleta ushindani.


Kotei ameeleza kuwa alikuwa na kazi kubwa ya kuzoea vyakula vya Tanzania lakini hicho kimepita bila kupingwa katika mwili wake.



“Napenda sana wali na maharage, hicho ndicho chakula ninachokipenda kwa hapa tangu nimefika,” alisema Kotei.

SOURCE: CHAMPIONI


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic