December 30, 2016



Kasi aliyoianza kiungo mshambuliaji mpya wa Yanga, Emmanuel Martin 'Mzenji', huenda ikawa tishio kwenye msimu huu wa Ligi Kuu Bara.


Kiungo huyo aliyewahi kuifunga Yanga kwenye mechi ya kirafiki, alitua kuichezea timu hiyo kwenye usajili wa dirisha dogo msimu huu akitokea JKU inayoshiriki Ligi Kuu ya Zanzibar.


Martin anayecheza nafasi ya kiungo mshambuliaji, alianza kucheza mechi yake ya kwanza ya ligi kuu dhidi ya African Lyon akitokea benchi na kumshawishi Kocha Mkuu wa Yanga, Mzambia, George Lwandamina kumuanzisha akicheza dakika 78 kabla ya kutolewa baada ya kuumia katika mchezo wa juzi dhidi ya Ndanda FC.


Alionyesha uwezo mzuri kwa kuwasumbua walinzi wa Ndanda kwa umahiri wa kukaa na kukokota mpira huku akiwapiga chenga mabeki na kutoa krosi safi.

Martin aliwapagawaisha mashabiki wa timu hiyo uwanjani, pale alipotoa pasi tatu za kichwa ndani ya 18 kwa Amissi Tambwe na Haruna Niyonzima waliopiga mashuti na kudakwa na kipa wa Ndanda, Jeremiah Kisubi.



Pia, kiungo huyo alifanikisha bao la tatu baada ya kupiga krosi safi kwa Tambwe ambaye alifunga katika dakika ya 25 na kuchangia Yanga kushinda mabao 4-0 katika mchezo huo. 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic