Wapenda soka la Italia keshokutwa Jumatatu watapata nafasi ya kutazama mechi ya Ligi Kuu ya Italia ‘Serie A’ kati ya Roma na AC Milan kupitia King’amuzi cha StarTimes Chaneli ya World Football.
Hii ni nafasi nyingine kwa mashabiki wa soka nchini na Afrika nzima kutazama mchezo huo mkali na wa aina yake utakaochezwa kwenye Uwanja wa Olimpico, kutokana na historia ya timu hizo kila zinapokutana.
Mshindi katika mchezo huo atakuwa amejiweka katika nafasi nzuri ya kuwania ubingwa wa Serie A dhidi ya Juventus iliyo kileleni ikiwa na pointi 36 wakati Milan na Roma zikiwa na pointi 32.
Wakati Kocha wa Roma, Luciano Spalletti akiwategemea zaidi Edin Dzeko na Mohamed Salah, Milan itakuwa na ukuta imara wenye nyota kama Mattia De Sciglio, Alessio Romagnoli, Ignazio Abate na kipa Gianluigi Donnarumma.
Mkuu wa Chaneli za Michezo za StarTimes, Muke Mwai Mugo, alisema anaamini Donnarumma atafanya vizuri.
“Ana umri wa miaka 17 tu, lakini Donnarumma anacheza kwa kujiamini akiweza kumiliki tofauti zote. Huyu anaelekea kuwa kipa nyota mpya duniani,” alisema Mugo.
Watazamaji wa Afrika watapata nafasi ya kumtazama Donarumma atakavyoweza kujaribu kuizuia ngome imara ya ushambuliaji ya Roma ambayo mpaka sasa imefunga mabao 35 wakati Milan inayo 27.
Huu ni moja kati michezo kumi ya Serie A ambayo itaonyeshwa kati ya Jumamosi, Jumapili na Jumatatu.
0 COMMENTS:
Post a Comment