December 10, 2016

KIMENYA AKITHIBITI MPIRA MBELE YA HARUNA NIYONZIMA WA YANGA


Klabu ya Simba inamtaka beki wa kulia wa Prisons, Salum Kimenya na hii si mara ya kwanza, sasa wanavutana kwani beki huyo anataka dau la Sh milioni 80 lakini Simba inazo Sh milioni 30 tu. Wamekwamia hapo.

Mabeki wa zamani wa Simba na Yanga, Boniface Pawasa na Bakari Malima wameipa Simba mchongo kuwa, kama wakimpata beki huyo mambo yao yatakuwa mazuri hata kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara.

Ni hivi, Simba inataka kumaliza tatizo la beki wa kulia kwani ina mpango wa kumtumia Janivier Bokungu kama beki wa kati kutoka kulia japokuwa taarifa zaidi zinasema pia inaweza kumtema mkabaji huyo.

Kimenya yeye anasisitiza kuwa ni mwajiriwa wa Jeshi la Magereza hivyo ili ajiunge na Simba ni lazima aiteme ajira yake ndiyo maana anataka dau la Sh milioni 80 vinginevyo hawezi kuchezea ajira yake.

Akizungumza na Kimenya alisema; “Unajua mimi hapa Prisons nipo kwenye ajira, siwezi kuacha kazi yangu kwa Sh milioni 30 yaani nitakuwa nimefanya kosa kubwa sana.

“Sitaki yanikute yaliyowakuta baadhi ya wachezaji walioacha kazi hapa na kwenda kujiunga na hizo timu, naweza kuacha kazi halafu huko nikakaa msimu mmoja, unaofuata nikafungashiwa virago, sasa nitakuwa nimefanya nini?

“Kama Simba wananitaka kweli wanipate fedha nzuri nikawafanyie kazi ambayo wataridhika nayo,” alisema Kimenya.

Wakizungumza kwa nyakati tokfauti, beki wa zamani wa Simba, Boniface Pawasa na yule wa Yanga, Bakari Malima walisema kuwa kama kweli Simba wana nia ya kumsajili Kimenya basi wafanye kweli kwani atawasaidia kwa kiasi kikubwa.

“Binafsi namjua vizuri sana Kimenya, nimekuwa nikimfuatilia kwa karibu sana, ni mchezaji mzuri ambaye uchezaji wake ni kama wa Shadrack Nsajigwa, siyo mtu wa kutaka tamaa pia ni mpambanaji anayetaka ushindi muda wote,” alisema Pawasa ambaye pia ni mchambuzi wa michezo katika gazeti la Championi.

Kwa upande wake Malima ambaye pia ni mchambuzi katika gazeti hili, alisema: “Kimenya ni beki mzuri pia ana uwezo wa kucheza nafasi nyingi uwanjani, kama Simba wanataka kumsajili, binafsi nawashauri wafanye kweli atawasaidia sana.”

Simba wamekuwa wakifanya siri kuhusu mipango yao ya kumsajili Kimenya ambaye anamaliza mkataba mwishoni mwa msimu huu.

SOURCE: CHAMPIONI 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic