January 10, 2017
Azam FC imetinga fainali ya Kombe la Mapinduzi baada ya kuitwanga Taifa Jang’ombe kwa bao 1-0.

Katika mechi hiyo iliyomalizika hivi punde kwenye Uwanja wa Amaan mjini Zanzibar, Azam FC walicheza vizuri lakini walipoteza nafasi nyingi.

Lakini Franka Domayo ‘Chumvi’ ndiye alifunga bao safi kwa shuti kali nje ya 18 akifunga bao hilo katika dakika ya 33. Domayo, kiungo wa zamani wa Yanga, ndiye ameibuka kuwa nyota wa mchezo huo.Azam FC ingeweza kupata mabao zaidi, lakini washambuliaji wake hawakuwa makini katika umaliziaji.

Hata hivyo, Taifa Jang’ombe walitoa upinzani kuanzia dakika ya kwanza hadi 90 wakionyesha wakati wowote wangeweza kusawazisha.
0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV