Mshambuliaji Amissi Tambwe wa Yanga alilambwa kadi ya njano baada ya kuifungia timu yake bao katika mechi dhidi ya Ndanda juzi kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar.
Tambwe alikumbana na kadi hiyo baada ya kufunga bao safi kabisa, lakini wakati anakwenda kushangilia akakirukia kibendera na kukipiga teke, kikavunjika.
Diego Costa wa Chelsea, naye ameendelea kukirukia kibendera kwa mara nyingine baada ya kuifungia timu yake dhidi ya Chelsea katika ushindi wa mabao 4-2.
Kibendera alichokirukia Costa hakikuvunjika maana si cha Mchina. Lakini kile alichokirukia Tambwe wakati Yanga iliposhinda 4-0. Mh!








0 COMMENTS:
Post a Comment