January 31, 2017Katibu Mkuu mpya wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa ameahidi kutoa ushirikiano kila nyanja katika klabu hiyo na kusisitiza hajastaafu ukocha.

Mkwasa amesema ataendelea kushirikiana na makocha wa Yanga akiwemo George Lwandamina.

Lakini angependa kufanya kazi ya ukocha kama vile kuzifundisha timu za vijana chini ya miaka 20 za Yanga.

“Ningependa kuendelea kufanya kazi yangu ya ukocha. Kuna timu za vijana, pia nitatoa ushirikiano kwenye benchi la ufundi la Yanga.

“Naushuru uongozi wa Yanga kwa kutambua mchango wangu pia, jambo ambalo litawahamasisha na wachezaji wengine wa zamani kuendelea kujituma na kufanya kazi zao kwa ufasaha,” alisema Mkwasa.


Baraka Deusdedit ndiye alikuwa akikaimu nafasi hiyo ya ukatibu mkuu hadi Yanga ilipomtangaza Mkwasa, leo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV