January 31, 2017




Baada ya kikosi cha Simba kutoa nje kucheza na Mamelodi, ssa timu hiyo itashuka dimbani Alhamisi, kuivaa Azam FC.

Taarifa zinasema, Mamelodi wataendelea na maandalizi kwa ajili ya mechi dhidi ya Azam FC hiyo Alhamisi, mechi inayotarajiwa kupigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi.

Awali, Mabingwa hao wa Afrika walitakiwa kucheza kesho dhidi ya Simba, lakini klabu hiyo imeona ina majukumu ya maandalizi dhidi ya Majimaji mjini Songea, wikiendi hii.


Lakini pia kumekuwa na taarifa kwamba waandaaji wa mechi hiyo hawakuwa na maandalizi mazuri kati yao na uongozi wa Simba kuhusiana na mechi hiyo.



Hata hivyo, mmoja wa waandaaji amesema, Simba walikuwa na taarifa za kutosha lakini wamegeuka huenda inatokana na wao kupoteza mechi dhidi ya Azam FC Jumamosi na Yanga ikaishinda Mwadui FC na kukwea kileleni.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic