January 31, 2017
Kama unakumbuka Bailey amekuwa ni pacha wa Mtanzania Mbwana Samatta.

Leverkusen imemwaga dola milioni 21 kumpata mshambuliaji huyo kinda matata wa Genk.
Samatta na Bailey mara kadhaa wamekuwa wakiisaidia Genk kupaa kwa kufunga au kutengeneza mabao muhimu. Kuondoka kwake kunakuwa na faida mbili kwa Samatta.

Kwanza atapata nafasi pana zaidi ya kucheza lakini kwa kuwa Bailey ametokea Genk maana yake timu nyingine za Ujerumani au nje ya Ujerumani, yaani sehemu nyingine barani Ulaya zitatupa jicho katika klabu hiyo.


Samatta ana uwezo mkubwa lakini hakuwa amepata nafasi ya kutosha akiwa Genk. Sasa anaweza kupata nafasi zaidi ili kuonyesha alichonacho na huenda ananukia kwenda mbali zaidi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV