January 31, 2017


Mabondia maarufu wa uzito wa juu mkongwe Wladimir Klitschko na Anthony Joshua sasa watakutana Aprili 29.

Mabondia hao watapigana kwenye Uwanja wa Wembley jijini London nchini Uingereza huku ikitarajiwa watu 90,000 watalishuhudia pambano hilo uwanjani hapo.

Watakuwa wakiwania mikanda ya IBF, IBO na  WBA yote ikiwa ni ya uzito wa juu.


Wamekutana jijini New York na kila mmoja ameonyesha mbwembwe na kujiamini kwamba atashinda.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV