January 5, 2017


Kiungo wa Simba ambaye anaendelea kufanya vizuri, Muzamiru Yassin amesema anatamani kuendelea kufunga mabao.
Muzamiru ambaye amekuwa kiungo mwenye kasi nzuri ya kufunga katika kikosi cha Simba, amesema angependa kuendelea kupachika mabao.

“Nafurahia kufunga, ningetamani niendelee kufanya vizuri kwa kufunga na kuisaidia Simba,” alisema.
“Lakini ikitokea sijafunga, ningependa kutoa pasi kwa wenzangu wafunge kwa kuwa ushindi ni wa kikosi chote.”

Muzamiru ambaye alijiunga na Simba akitokea Mtibwa Sugar ameonyesha uwezo mkubwa katika upachikaji mabao lakini ni sehemu ya msaada mkubwa Simba.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV