January 1, 2017



Mabao ya Juma Luizio na Muzamiru Yassin yameifanya Simba kuanza vema michuano ya Mapinduzi.

Simba imeitwanga Taifa Jang’ombe kwa mabao 2-1 katika mechezo wake wa kwanza wa michuano hiyo kwenye Uwanja wa Amaan mjini Zanzibar.

Simba walikuwa wa kwanza kupata bao kupiitia Muzamiru katika dakika ya 28 ambaye aliuwahi mpira uliotemwa na kipa na kuukwamisha kambani.

Ikionekana kama timu hizo zitaenda mapumziko Simba ikiongoza kwa bao 1-0, Luizio alipachika bao la pili akiwa katikati ya msimu wa mabeki wa Taifa.

Kipindi cha pili kilionekana kina mashambulizi mengi ya kupokezana lakini beki wa Simba, Noverty Lufunga ‘alichafua gazeti’ baada ya kujifunga akiunganisha langoni mwake mpira wa kona.

Simba ingeweza kupata mabao mengi zaidi kama washambuliaji wake wangekuwa makini katika umaliziaji.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic