Kiungo wa bei kubwa wa Manchester United, Paul Pogba anaweza kuingia
matatani baada ya kuonekana akiendesha gari huku akitumia simu kitu
ambacho ni kinyume na sheria za uendeshaji gari nchini England.
Pogba ameonekana akiendesha gari lake aina ya ua Audi RS6-R lenye thamani ya pauni 85,000 alipokuwa akiwasili mazoezini kwenye Uwanja wa Carrington, Ijumaa iliyopita.
Picha zimemuonyesha akiwa ameishika simu yake hiyo huku akiendesha gari na kama mamlaka husika za usalama barabarani zitaamua kutumia picha hiyo zinaweza kumuingiza matatizoni.
0 COMMENTS:
Post a Comment