January 15, 2017Kikosi cha Yanga kimeishasahau kabisa masuala ya Kombe la Mapinduzi na nguvu zimeelekezwa kwenye Ligi Kuu Bara.

Meneja wa Yanga, Hafidhi Saleh amesema wamerejea na kuendelea na maandalizi kwa ajili ya Ligi Kuu Bara ambayo wao ni watetezi.

“Tunajua Majimaji ni timu ngumu kwetu, lakini tunataka pointi tatu na sasa nguvu zetu ni kwenye ligi kuu,” alisema.

Yanga inasafiri kwenda kuivaa Majimaji kwao Songea, Jumanne.


Huo utakuwa ni mchezo wa kwanza baada ya kurejea kutoka Zanzibar kwenye michuano ya Mapinduzi Cup ambako waling’olewa kwenye nusu fainali na watani wao Simba kwa mikwaju ya penalti 4-2.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV