January 2, 2017Mabingwa wa soka Tanzania Bara, Yanga wameanza michuano ya Mapinduzi Cup kwa kishindo kwa kuwachapa Jamhuri kwa mabao 6-0.

Katika mechi hiyo iliyochezwa kwenye Uwanja wa Amaan mjini Zanzibar, leo. Yanga ndiyo walitawala mchezo huo kwa kiwango kikubwa.

Mzimbabwe Donald Ngoma alifunga mabao mawili kama ilivyokuwa kwa Simon Msuva ambaye alicheza vizuri mechi hiyo.

Mzimbabwe mwingine, Thabani Kamusoko alifunga bao moja kama ilivyokuwa kwa Juma Mahadhi ambaye aliingia katika kipindi cha pili.
Yanga ilipata bahati mbaya baada ya kiungo wake, Justice Zulu kuumia na kushonwa nyuzi nne baada ya kugongana na mchezaji wa Jamhuri wakiwania mpira.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV