January 4, 2017Kikosi cha Yanga kimeendelea kuchanja mbuga katika michuano ya Kombe la Mapinduzi baada ya kuitwanga Zimamoto kwa mabao 2-0.

Katika mechi hiyo kwenye Uwanja wa Amaan mjini Zanzibar, leo. Yanga walitawala kila idara huku Zimamoto wakionekana kuwa na hofu kuu dhidi ya mabingwa hao wa Tanzania Bara.

Simon Msuva ndiye alikuwa shujaa wa Yanga baada ya kufunga mabao yote mawili.

Hata hivyo, Msuva alikosa mkwaju wa penalti katika dakika ya 50, baada ya kupiga kipa akapangua, alipouwahi na kupiga tena ukagonga mtambaa wa panya na kipa akaudaka.


Hiyo ilikuwa ni mechi ya pili ya Yanga katika michuano ya Mapinduzi na sasa imefikisha pointi sita na mabao nane katika mechi hizo mbili.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV