Mratibu wa Mtibwa Sugar, Jamal Bayser amesema kubadili makocha mfululizo, kumechangia wao kuteteleka msimu huu.
Lakini amesisitiza, wataendelea kufanya maandalizi sahihi ili kufanya vizuri katika mechi zilizobaki.
Bayser amesema kuondoka kwa Mecky Maxime aliyekwenda Kagera Sugar, baadaye wakamchukua Salum Mayanga ambaye amechukuliwa kuinoa Taifa Stars.
"Sasa utaona kuna kocha mwingine tena. Hivyo ni jambo la kuvuta subira na tunalazimika kuendelea kufanya maandalizi ya kutosha," alisema.
Katika msimamo wa Ligi Kuu Bara ambao Simba ni vinara, Mtibwa Sugar iko katika nafasi ya 5 wakiwa na pointi 32.
0 COMMENTS:
Post a Comment