Katibu Mkuu wa zamani wa Simba, Mwina Seif Kaduguda, jana alijikuta akitembea kwa miguu kutoka Uwanja wa Taifa hadi kwake Gongolamboto jijini Dar es Salaam.
Kutoka Uwanja wa Taifa hadi Gongolamboto ni takribani kilomita tisa hadi kumi, lakini Kaduguda alitembea bila ya kuchoka akisema ilikuwa ni furaha ya ushindi dhidi ya Yanga.
Simba iliifunga Yanga kwa mabao 2-1 ikiwa pungufu baada ya Bésala Bukungu kulambwa kadi nyekundu. Mabao ya Simba katika mechi hiyo yalifungwa na Laudit Mavugo na Shiza Kichuya.
Kaduguda ambaye ni mwalimu wa Sekondari ya Jitegemee, amesema alitembea hadi Gongolamboto na hakuchoka.
“Furaha ni kitu cha aina yake, nilijikuta nikipiga mguu tu hadi nyumbani. Taifa hadi Gongolambo ni mbali sana lakini hauchoki.
“Hakuna furaha kama kuifunga Yanga, hivyo ilikuwa siku nzuri. Lakini sasa ni vizuri kujipanga kuhakikisha kunakuwa na umoja na timu ifanye vizuri zaidi,” alisema Kaduguda ambaye pia aliwahi kuwa kocha msaidizi wa Simba.
0 COMMENTS:
Post a Comment