February 13, 2017

Kutokana na mwenendo wa Leicester City kuendelea kuwa mbaya, beki wa zamani wa Arsenal, Martin Keown amedai kuwa kiungo mshambuliaji wa Leicester City, Riyad Mahrez ameshindwa kung’ara hivi karibuni kutokana na kuonyesha tabia za uvivu.
Riyad MahrezAkizungumza kama mchambuzi wa soka kwenye runinga Keown alisema anaamini Leicester imeshindwa kuwika msimu huu kama ilivyokuwa msimu uliopita kutokana na wachezaji wa timu hiyo kutoonyesha bidii.

Mahrez alikuwemo katika kikosi kilichofungwa 2-0 na Swansea, jana huku akishindwa kuonyesha ubora kama ilivyokuwa msimu uliopita na kuifanya timu hiyo sasa kuwa hatarini kushuka daraja.

Martin Keown
“Alikuwa na uwezo wa kuwasumbua wapinzani anavyotaka, hilo sasa halifanyiki kwa kuwa kuna uvivu fulani na haonyeshi kama anataka hilo litokee,” alisema Keown.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV