February 13, 2017

Februari 2016 dunia ilishuhudia Ligi Kuu ya China ikipata mchezaji mpya kutoka Ulaya katika dili la kihistoria, ambapo Klabu ya Hebei China Fortune ilimsajili Ezequiel Lavezzi kutoka Paris Saint-Germain ya Ufaransa, lakini sasa hali ya mambo imekuwa ndivyo sivyo.

 
Mchezaji huyo ambaye ni mshambuliaji, akiwa na umri wa miaka 30 wakati huo alisajiliwa kwa pauni milioni 23.5 na kusababisha mitandao ya jamii ya China kumtamka kuwa atakuwa Maradona wao mpya kwa kuwa naye ni raia wa Argentina.

Leo umetimia mwaka mmoja tangu usajili huo ukamilikwe lakini mchezaji huyo hajafunga bao hata moja licha ya kuwa mshshara wake unatajwa kuwa ni pauni 493,000 (zaidi ya shilingi bilioni 1) kwa wiki, akiwa pia amekabidhiwa nyumba mbili za kuishi,magari mawili, mpishi na dereva.

Mpaka sasa Lavezzi amecheza mechi 10 tu tangu asajiliwe na akiwa ametoa pasi tatu za bao huku muda mwingi akitumia kuwa nje kwa kuwa aliumia mkono na akatakiwa kufanyiwa upasuaji.


Aliumia mkono Mei katika michuano ya Copa America alipokuwa kiitumikia Argentina na tangu hapo amekosa mechi nyingi za ligi ya China.

REKODI ZA EZEQUIEL LAVEZZI
2003–04: Estudiantes 39 (17 goals)
2004: Genoa 0 (0 goals)
2004–07: San Lorenzo 84 (25 goals)
2007–12: Napoli 156 (38 goals)
2012–16: PSG 107 (22 goals)
2016–: Hebei Fortune 10 (0 goals)

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV