Kiungo wa zamani wa Yanga, Godfrey Bonny amefariki dunia, baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Bonny maarufu kama Ndanje, amefariki dunia baada ya kulazwa muda mrefu katika Hospitali ya Makandana, Tukuyu mkoani Mbeya.
Nahodha wa zamani wa Yanga, Shadrack Nsajigwa ambaye alikuwa nahodha wakati Bonny akiichezea Yanga, amethibitisha taarifa hizo.
“Kweli nimepokea taarifa hizi za masikitiko, ndugu yetu ametangulia mbele za haki. Juhudi zilifanyika lakini Mungu alishapanga,” alisema.
Kiungo huyo aliichezea Yanga kwa kiwango kikubwa akitokea Prisons.
Baada ya kuondoka Yanga alikwenda nchini Nepal ambako alicheza soka la kulipwa akiwa na Watanzania wengine akiwemo Nsajigwa.
Mwenyezi Mungu Ampumzishe kwa Amani
0 COMMENTS:
Post a Comment