Mtanzania Mbwana Samatta amecheza kwa dakika 90 wakati timu yake ya Genk ikipata sare ya mabao 2-2 dhidi ya Astra Giurgiu katika mechi ya Kombe la Europa.
Giurgiu ilikuwa nyumbani na ndiyo ilialazimisha kusawazisha bao kupitia Constantin Badescu katika dakika ya 43.
Hii ilikuwa baada ya Genk kupata bao la kwanza katika dakika ya 25 kupitia Timothy Castagne.
Genk waliongeza bao la pili dakika ya 83 mfungaji akiwa Leandro Trossard.
Ikionekana kama walikuwa wameshinda, Takayuki Seto akatibua sherehe baada ya kuifungia Astra bao la kusawazisha katika dakika ya 90.
0 COMMENTS:
Post a Comment