February 27, 2017



Ushindi una raha yake na mastaa wa Simba hivi sasa wanatembea kifua mbele kutokana na kufurahiwa na kila mdau wa timu hiyo lakini juzi walipewa mamilioni ya tajiri Mohamed Dewji ‘Mo’ huku viongozi wengine wa klabu hiyo nao wakiwamwagia mamilioni mengine.

Raha yote hiyo inatokana na kuifunga Yanga mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, juzi na kujikita kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo kwa tofauti ya pointi tano.

Habari kutoka ndani ya Simba, zimedai kuwa, juzi Jumamosi kabla ya mchezo huo, wachezaji hao walipewa Sh 5,000,000 kutoka kwa Mo wagawane lakini pia wakaahidiwa Sh milioni 15 za papo kwa papo kama wataifunga Yanga.

Mmoja wa viongozi wa timu hiyo ambaye aliomba kutotajwa jina lake alisema: “Hali hiyo iliwafanya wachezaji wapambane vilivyo uwanjani na baada tu ya mechi hiyo walipewa fedha zao hizo milioni 15 na kugawana.

“Lakini pia leo hii kuna milioni 15 nyingine watapewa watakapokutana na uongozi kwa lengo la kuwapongeza kutokana na kazi yao kubwa waliyoifanya uwanjani jana (juzi) lakini pia kuna uwezekano pia mwanachama wetu Mohamed Dewji naye akatoa kiasi kama hicho cha fedha kwani pia aliahidi kuwashangaza wachezaji wetu kama wataifunga Yanga,” kilisema chanzo hicho cha habari.

Katika hatua nyingine kikosi hicho cha Simba leo hii asubuhi kitaendelea na mazoezi yake ya kujiandaa na mechi zake za ligi kuu pamoja na Kombe la FA zilizobakia.

Kocha Mkuu wa Simba, Mcameroon, Joseph Omog, amesema mazoezi hayo yatafanyika katika Uwanja wa Chuo Kikuu cha Polisi, Kurasini jijini Dar es Salaam.


SOURCE: CHAMIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic