February 27, 2017


Mshambuliaji nyota wa Simba, Mrundi, Laudit Mavugo, ameweka bayana kwamba, sasa ubingwa upo wazi kwa upande wao, baada ya kuwafunga wapinzani wao, Yanga na kufikisha gepu la pointi tano mbele yao, jambo ambalo linawafanya kuendelea kung’ang’ania kileleni.

Mavugo alichangia kwa kiasi kikubwa ushindi wa Simba wa mabao 2-1 dhidi ya Yanga kwenye mechi ya ligi kuu iliyopigwa Uwanja wa Taifa, Dar. Bao lingine la Simba lilifungwa na Shiza Kichuya na Yanga wao walifunga kupitia kwa Simon Msuva.

Mavugo amesema kwamba njia ya ubingwa ipo wazi kwa kuwa Yanga ndiyo ilikuwa timu pekee ambayo waliifikiria inaweza kuharibu mipango yao lakini baada ya kuifunga hakuna ambaye anaweza kuwazuia tena.

“Hakuna ambaye anaweza kutuzuia tena baada ya kuifunga Yanga kwa sababu wao ndiyo walikuwa wapinzani wetu na ambao tulikuwa tukiwahofia kwamba wanaweza kutuvurugia malengo yetu ya kuwapa ubingwa mashabiki ambao wamekuwa wakiungojea kwa hamu.

“Kilichobaki ni kushinda mechi hizi saba zilizobakia na tunajua hakuna ambaye atatuzuia kushinda kwa sababu sisi ni bora na tuna muunganiko mzuri ambao ndiyo unachangia kwa kiasi kikubwa kushinda mechi zetu,” alisema Mavugo.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic