February 4, 2017


MPIRA UMEKWISHAAAA
DAKIKA 3 ZA NYONGEZA
Dk 90, Muzamiru yuko chini pale na wauguzi wanaingia kumhudumia
Dk 89, krosi nzuri hapa kwenye lango la Simba lakini Bukungu anaokoa

GOOOOOOOO Dk 88, Mavugo anamchambua Saleh Mohamed ndani ya 18 na kuachia mkwaju safi
 Dk 87, mpira mzuri wa faulo wa DK 85, Agyei anafanya kazi nyingine nzuri, anatoka na kupangua mpira kichwani kwa Mpole
SUB Dk 73, Majimaji wanamtoa Kibuta wanamuingiza George MpoleDk 82, anafanya kazi kubwa ya kuokoa mkwaju wa Hamisi, lilikuwa shuti linalokenda langoni


Dk 81 sasa, inaonekana Simba wanaimarisha ulinzi huku wakifanya mashambulizi ya kushitukiza. Hata hivyo wachezaji wake kadhaa wanaonekana kutoimarika katika ukabaji
Dk 76, mpira wa adhabu, Sabato anaachia mkwaju mkali lakini hakulenga lango
SUB Dk 76, Simba wanamtoa Ndemla na nagasi yake inachukuliwana Mwinyi Kazimoto
SUB Dk 73, Majimaji wanamuingiza Lucas Kikoti kuchukua nafasi ya Marceil Kaheza
Dk 73, Sabato anajaribu tena shuti kali lakini hakulenga lango


KADI Dk 71, kadi ya kwanza ya mchezo huu inakwenda kwa Muzamiru baada ya kucheza kindava
Dk 70 sasa, zimebaki dakika 20 na Simba wanaonekana kurudi nyuma huku wakifanya mashambulizi ya mipira mirefu
Dk 68, Majimaji wanapata kona ena baada ya krosi ya Saleh Mohammed kuokolewa
GOOOOOOOOO Dk 64 Ndemla anaachia mkwaju mkali na kuiandikia Simba bao la pili. Ulikuwa ni mpira safi wa kona, Majimaji wakajichanganya naye hakufanya ajizi


Dk 63, Simba wanagongeana vizuri, Mavugo anampa Kotei anaachia shuti kali, linaokolewa na kuwa kona
SUB DK 60, James Kotei anaingia kuchukua nafasi ya Ajibu, mfungaji wa bao pekee hadi sasa
Dk 58, Mavugo anamchambua beki hapa, anaachia mkwaju lakini hakulenga langoDk 57 sasa, Majimaji ndiyo wanaoshambulia sana, Simba wanapaswa kuwa makini kwa kuwa inaweza kuwa hatari kwao
Dk 56, Kaheza, yeye na kipa anapiga lakini mpira wake unamgonga kipa na kwenda nje. Kona, inachongwa lakini haina faisa


DK 52, mpira mzuri wa Mavugo unaokolewa na kuwa kona, inachongwa na kuzaa kona nyingine
SUB Dk 52, Simba wanamtoa Juma Liuzio na nafasi yake inachukuliwa na Pastory Athanas
Dk 50, Sabato anajaribu kumtoka Mwanjale lakini anautoa na kuwa kona, inachongwa, Agyei anapangua na mabeki wanaondosha
Dk 49, Kibuta anageuka na kuachia mkwaju mkali kwa mara nyingine, lakini hakulenga lango. Goal kick
Dk 47 Simba wanagongeana vizuri kabisa hapa na Ajibu anaachia mkwaju mkali kabisa lakini sentimeta chache, goal kick
Dk 45, mechi imeanza kwa kasi na Simba wanakuwa wa kwanza kufika kwenye lango la Majimaji
MAPUMZIKO
Dk 45+1 shuti la mpira wa adhabu wa Kaheza, Agyei anatema na mabeki wake wanaokoa. Inakuwa kona lakini haina manufaa kwa Majimaji
DK 45+1, krosi nzuri kabisa, Kibuta yeye na kipa wa Simba, anafumba macho na kuukosa mpira

DAKIKA 1 YA NYONGEZA
Dk 45, Majimaji wanaingia tena kwenye lango la Simba lakini Mwanjale anaokoa mbali kabisa
DK 44, nafasi nzuri kwa Majimaji, Sabato anaupata vizuri anapiga kichwa lakini anashindwa kulenga
DK 42 sasa, Majimaji wanaonekana kufunguka na kucheza vizuri lakini hawako makini sana wanapoingia kwenye lango la Simba
Dk 40, Kipangile wa Majimaji anaingia kwenye lango la Simba, lakini anashindwa kutulia
Dk 39, Selemani Kibuta mbele ya Muzamiru anaachia mkwaju mkali kabisa hapa, unatoka pembeni kidogo ya lango la Simba
Dk 35, Mavugo anapokea pasi nzuri ya Ajibu na kupiga shuti kali, linatoka sentimeta chache kabisa
Dk 31, Sabato anaingia vizuri tena na kuachia shuti lakini hakulenga
Dk 28 Majimaji wanapoteza nafasu nzuri hapa na Agyei anadaka vizuri kabisa


Dk 22, Sabato anapoteza nafasi nzuri baada ya kuunganisha kichwa karibu na lango la Majimaji lakini hakulenga
GOOOOOOO Dk 19, krosi safi ya Shiza Kichuya, Ajibu anaunganisha vizuri kwa kichwa na kuandika bao la kwanza kwa Simba
Dk 15 sasa, Simba wanaonekana na kugongeana vizuri lakini bado hakuna kashkash kubwa wanayofikisha langoni
Dk 12, Kona ya pili wanapata Majimaji hapa baada ya Bukungu kuutoa mpira nje, inachongwa lakini Agyei anadaka
Dk 11 Simba wanagongeana vizuri na Liuzio anaupachika mpira wavuni. Mwamuzi anasema kabla, tayari alikuwa ameotea
DK 9, krosi inapigwa langoni mwa Simba, kipa Agyei anakwenda markiti lakini Zimbwe au Tshabalala anajitokeza na kuokoa vizuri kabisa


Dk 8, kona ya kwanza ya mchezo wanapata Majimaji baada ya Mwanjale kuutoa mpira kwa kichwa
Dk 7, Peter anageuka na kuachia mkwaju hapa lakini Agyei anadaka kwa ulaini
Dk 7 sasa, bado mpira unachezwa zaidi katikati ya uwanja na hakuna mashambulizi makubwa ndani ya 
Dk 2 Simba wanaingia kwenye lango la Majimaji, Mazamiru anapiga shuti linawababatiza mabeki hapa na wanaokoa
Dk ya 1, Majimaji wanaanza kwa kasi, krosi nzuri inapigwa hapa lakini mwamuzi anasema offsideKIKOSI CHA SIMBA:
1. Daniel Agyei
2. Janvier Bukungu
3. Mohamed Zimbwe
4. Novatus Lufunga
5. Method Mwanjale (C)
6. Muzamiru Yassin
7. Shiza Kichuya
8. Said Ndemla
9. Laudit Mavugo
10. Juma Liuzio
11. Ibrahim Ajibu

SUB
Peter Manyika
Mwinyi Mazimoto
James Kotei
Haji Ugando
Athanas 

Kitandu

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV