February 11, 2017


MPIRA UMEKWISHAAAA
DAKIKA 4 ZA NYONGEZA
Dk 90, Bado Simba wanagongeana zaidi mpira katikati ya uwanja
Dk 86 hali inavyokwenda inaonekana Simba wameridhika na wanajaribu kujilinda
KADI Dk 83 Fabianka analambwa kadi ya njano kwa kumzuia kwa mkono Zimbwe. Ndiyo kadi ya kwanza ya njano katika mchezo huu
Dk 82, Kichuya anaaachia mkwaju mkali, kipa anaupangua lakini unagonga mwamba na kuokolewaDk 80, Pastory anaachia mkwaju hapa lakini inakuwa goal kick
SUB Dk 77 Salum Bosco anaingia kuchukua nafasi ya Victor Hangaya (Huyu ndiye aliifunga Simba mabao yote mawili kule Mbeya)


Dk 76, Prisons wanapata baada ya kusukuma shambulizi, lakini Pastory anasaidia hapa na kuokoa
SUB Dk 74 Pastory Athanas anaingia kuchukua nafasi ya Ibrahim Ajibu
Dk 73, Prisons wanaingia vizuri na Meshack anauchonga vizuri mpira lakini unatoka nje kidogo mwa lango la Simba
Dk 73, pasi nzuri ya Mavugo, Kazimoto anaachia shuti kali hapa, lakini kipa anadaka
Dk 72, Ndemla anaachia shuti kali hapa lakini goal kick
SUB Dk 70 Shiza Kichuya anaingia kuchukua nafasi ya Liuzio
GOOOOOOO Dk 68, Mavugo anaifungia Simba bao la tatu kwa Kichwa akiunganisha krosi ya outer ya Ajibu
Dk 65 Chona wa Prisons naye yuko chini paleSUB Dk 62, Kazimoto anaingia kuchukua nafasi ya Mwanjale 
Dk 62 Mwanjale anatolewa nje kwenda kutibiwa


Dk 61, Mwanjale yuko chini baada ya kuumia, inaonekana hataendelea kwani mara ya pili ndani ya dakika 5 anaanguka na kutibiwa
Dk 58, Agyei tena anaikoa Simba baada ya krosi dongo ya Kimenya
Dk 57, Krosi ya Bukungu ndani ya eneo la hatari lakini haikumfikia yoyote, Prisons wanaokoa
SUB Dk 56 upande wa Prisons Meshack Selemani anaingia kuchukua nafasi ya Benjamin Asukile
Dk 55, Mavugo anawatoka mabeki wa Simba, wanaokoa na kuwa kona, inachongwa lakini goal kick


Dk 54, Prisons wanaingia ndani ya eneo la hatari la Simba, Agyei anafanya kazi ya ziada tena
Dk 51, krosi nzuri ya Kimenya ndani ya lango la Simba, Agyei anatokea na kudaka kama nyani
Dk 49, Hamisi wa Prisons anageuka vizuri na kuachia mkwaju lakini unakuwa goal kick
Dk 47, Mwanjale anafanya kazi ya ziada kuokoa mbele ya Asukile aliyekuwa anakwenda kumuona Agyei, yuko chini anatibiwa sasa
Dk 45, kipindi cha pili kimeanza na kila upande unaonekana kuwa makini

(Kwa ilivyokuwa, kama mwamuzi Mahagi alimaliza dakika 45 za kwanza kabla)MAPUMZIKO
Dk 44 Simba wanaendelea kushambulia mfululizo lakini Prisons wanaonekana kucheza kazikazi
Dk 41, jaribio jingine zuri la Prisons lakini Agyei anatokea na kuokoa
Dk 40, Prisons wanagongeana vizuri na mpira unamkuta Kimenya anaachia mkwaju mkali kwelikweli lakini hakulenga lango


SUB Dk 38 Kassim Njinyaji anaingia kuchukua nafasi ya Kazungu upande wa PrisonsDk 36, mita 28, Ndemla anaamua kugeaka na kuachia mkwaju lakini halikulenga lango
Dk 35, Mavugo naye anajipindua na kupiga teke la baiskeli lakini hakulenga lango
Dk 35, Hangaya anapiga tik tak lakini mguu wake unamgonga Mwanjale na mwamuzi anasema faulooo
Dk 33, mkwaju wa faulo unaingizwa kwenye lango la Simba lakini Agyei aruka juu na kudaka vizuri
Dk 31, Simba wanagongeana vizuri hapa na Muzamiru anageuka na kuachia shuti lakini halikuwa kali
GOOOOOOO Dk 28 Ajibu anapokea pasi nzuri ya Mavugo, naye anamchambua kipa wa Prisons kama penalti na kuandika bao safi kabisa

Dk 28 sasa, mpira zaidi unachezwa katikati ya uwanja huku Prisons wanajilinda sana
Dk 23, Asukile anaingia vizuri, anamtoka kipa Agyei lakini mpira unaokolewa na kuwa kona ya kwanza ya Prisons lakini Agyei anadaka kwa ufundi hapa
Dk 20, Simba wanapata kona ya pili, inachongwa hapa na Mavugo anautupia mpira wavuni lakini kabla Liuzio alifanya faulo
GOOOOOOO DK 18, krosi ya Bukungu inagongwa na kumkuta Liuzio, anaweka kifuani na kuandika bao la kwanza kwa Simba leo na la kwanza kwake katika Ligi kuu Bara
Dk 17, kona ya kwanza ya mchezo wanapata Simba baada Prisons kuokoa

Dk 15, krosi nzuri ya Ajibu, Mavugo anaiwahi ndani ya 12 lakini mwamuzi anasema amecheza mashambi
Dk 12, Asukile anapiga kichwa hapa lakini hakulenga lango na inakuwa goal kick
Dk 10, Liuzio anaingia kwa kasi anatoa krosi hapa lakini Mpalile na wenzake wanaokoa hapa


Dk 7 sasa, mpira upo katikati zaidi huku Prisons wakiendelea kuwa nyuma zaidi wakilinda
Dk 5 sasa, Simba wanaonekana kuhamia kwenye lango la Prisons, lakini walinzi wa Prisons wanaonekana bado wako makini
Dk 3 anamchambua Mpalile, anaachia shuti lakini si kali na halikulenga lango
Dk 2, Ajibu anapokea pasi nzuri ya Ndemla lakini kipa anatokea na kuokoa vizuriii kabisa
Dk ya 1, Simba wanakuwa wa kwanza kufika katika lango la Prisons lakini kipa Aron Kalambo anadaka kwa ulaini

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV