February 9, 2017


Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji amewasili katika
kituo cha Kikuu cha Polisi cha Dar es Salaam akiongozana na mlinzi wake pamoja na baadhi ya mashabiki wa klabu ya Yanga.

Baadhi ya mashabiki hao waliongozana naye hadi katika lango la kuingilia kwenye kituo hicho ambako walipigwa stop na askari.


Manji aliahidi anakwenda leo kuhojiwa baada ya kuwa kwenye listi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda. 

Makonda alimtaka Manji kufika kituoni hapo kesho akiwa na watu wengine 64 waliotajwa kwenye listi wakituhumiwa kujihusisha, kujua taarifa au jambo fulani kuhusiana na madawa ya kulevya.
0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV