February 9, 2017

KIKOSI CHA PSIRONS


Prisons wamesema wako tayari kwa ajili ya mechi dhidi ya Simba, Jumamosi.

Kocha Mkuu wa timu hiyo, Abdallah Mohammed amesema wamejiandaa vilivyo kuhakikisha wanafanya vizuri na kuendeleza ubabe kwa Simba.

Katika mzunguko wa kwanza, Simba walilala kwa mabao 2-1 mjini Mbeya na Prisons ikawa timu ya pili kuifunga Simba msimu huu baada ya African Lyon.

“Tunajua Simba ni timu ngumu sana. Lakini tumejiandaa vizuri na tunataka ushindi,” alisema Mohammed.

“Hata kama kuna ugumu, tutapambana kuhakikisha tunafanya vizuri.”


Jana, Meneja wa Simba, Mussa Hassan Mgosi alisisitiza kwamba wako tayari kwa ajili ya mechi hiyo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV