February 23, 2017
Siku moja baada ya kampuni ya Tigo kuanza kuhaha mitandaoni ikikanusha kuwa kampuni hiyo haimilikiwi na kampuni ya Golden Globe inayomilikiwa na mfanyabiashara Yusuf Manji, Nankaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) imesimamisha mchakato wa kuingiza hisa za Tigo katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE).

Jana kulisambaa taarifa mitandaoni, Tigo ikipinga kwamba Tigo inamilikiwa na Manji. Hii ikiwa ni baada ya vyombo vya habari kueleza mfanyabiashara huyo alivyonunua kampuni hiyo namba mbili kwa ukubwa kwa zile za mawasiliano nchini.

Kawaida kampuni hutakiwa kujisajili kwa asilimia 25 ya hisa zake, hii ni kwa mujibu wa sheria.

Hadi sasa kuna kesi mahakamani, Golden Globe ya Manji ambayo iliinunua kampuni hiyo ilipopigwa mnada na Milcomn Tanzania NV ambao walikuwa wamiliki wa awali.


Kwenye mnada uluiofanywa chini ya usimamizi wa mahakama, Golden Globe iliinunua kampuni hiyo kwa asilimia 99, hivyo kumfanya Manji awe mmiliki mwenye hisa zote kasoro moja tu.


Msemaji wa CMSA, Charles Shirima amethibitisha kuondolewa kwa hisa za Tigo kutokana na mvutano huo ulio mahakamani kati ya kampuni ya Manji na wamiliki wa sasa ambao asili yao ni kampuni yenye mamao yake makuu nchijni Sweden.

Baada ya kuinunua Tigo Mahakamani na kukamilisha kila kitu cha umiliki Novemba 5, 2014, sasa Golden Globe inamiliki hisa 34,479 kati ya 34,480 na hisa moja iliyobaki inamilikiwa na kampuni ya Shai Holdings.

Hicho ndicho wanachopinga Milcomn Tanzania NV mahamani wakihoji utaratibu uliotumika kuinunua kampuni hiyo.

Hivyo Golden Globe imesimamisha mchakato huo wa usajili na baadaye uuzwaji wa hisa kwa kuwa yenyewe ndiye mmiliki wa kampuni ya Tigo kwa asilimia 99 na haikushirikishwa.

Tayari kuna taarifa kwamba, kupitia Golden Globe, klabu kongwe nchini ya Yanga itafaidika kwa kupata udhamini mnono wa mabilioni ya fedha hasa mara tu baada ya kesi hiyo kwisha na kama watakuwa wameshinda.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV