Kocha Mkuu wa Simba, Joseph Omog amekwenda anashusha ukali wa mazoezi ya kikosi chake.
Simba ipo kambini mjini Zanzibar kujiandaa na mechi ya Jumamosi dhidi ya watani wao Yanga.
Omog ameanza kupunguza ukali wa mazoezi na ndani ya siku hizi tatu, inaonekana watakuwa na mazoezi mara moja kwa siku badala ya mara mbili.
“Kweli kwa siku mazoezi yalikuwa ni siku mbili mfululizo, lakini sasa mazoezi yamekuwa mara moja kwa siku,” alisema mmoja wa wachezaji wa Simba.
“Tunaendelea vizuri sana kwa kweli, mazoezi mara moja kwa siku inaweza kuwa asubuhi pekee au jioni pekee.”
Katika mechi ya kwanza, Simba na Yanga zilimaliza kwa sare ya 1-1, Simba wakishawazisha dakika za mwishoni kwa bao la Shiza Kichuya ambaye alipiga mpira wa kona, ukajaa moja kwa moja wavuni.
0 COMMENTS:
Post a Comment