February 23, 2017


Kocha wa zamani wa Yanga, Tom Sanintfiet amesema binti yake Nikelwa ndiyo furaha yake namba moja hata kuliko mpira.

Saintfiet ambaye sasa ni Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya Trinidad and Tobago amesema binti huyo ndiyo mwenye miezi kadhaa tu, ndiyo raha yake kuu hata kuliko soka.


“Soka ni kazi yangu, furaha yangu. Lakini kwa sasa furaha namba moja ni Nikelwa, hilo halina mjadala,” alisema.

Yeye na mkewe walikaa miaka nane, kati ya hiyo minne wakiwa kama wapenzi na minne mingine kama mke na mume.

Saintfiet ambaye anapenda kucheza soka la kushambulia aliipa Yanga ubingwa wa Kombe la Kagame.


Lakini ni kocha amefundisha timu nyingi za taifa kama Malawi, Namibia, Ethiopia. Lakini amefundisha karibu mabara yote ya Afrika, Ulaya, Asia na Amerika. 





0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic