February 23, 2017



Mkuu wa Upelelezi wa Wilaya ya Kibiti, Mrakibu Msaidizi wa Polisi, Peter Kubezya aliyeuwawa na watu wanaoaminika huenda ni magaidi, alikuwa shabiki mkubwa wa Yanga.

Marehemu Kubezya alikuwa kati ya mashabiki wakubwa wa Yanga ambao ndiyo mabingwa watetezi wa Tanzania Bara.

Askari huyo aliuwawa katika opresheni maalum aliyokuwa akiiongoza katika enero Jaribu Mpakani wilayani Kibiti.

Tukio lilitokea katika kizuizi cha barabarani katika eneo hilo na aliwawa wakati wa majibizano na askari hao baada ya kupigwa risasi kiunoni.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Kamishna Msaidizi, Boniventure Mushongi alithibitisha kifo cha Kubezya ambaye hivi karibuni alihitimu elimu ya chuo kikuu.


Mwenyezi Mungu Amrehemu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic