February 27, 2017

MSUVA

Kiungo wa Simba, Mghana, James Kotei, amechungulia katika kikosi cha Yanga na kusema: “Simon Msuva ndiye mchezaji bora kwa upande wa Yanga.”  

Kotei ameyasema hayo baada ya kuisaidia timu yake ya Simba kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Yanga katika mchezo wa Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Taifa, Dar.

Kotei amesema ushindi walioupata dhidi ya Yanga haumaanishi kwamba wapinzani wao hawakuwa vizuri, bali waliwazidi kidogo na kutumia udhaifu wao.

KOTEI

“Yanga walikuwa wazuri na ndiyo maana waliweza kutufunga kabla ya sisi kusawazisha na kuwaongeza, kikubwa pointi tatu tulizozipata ni juhudi zetu binafsi hasa ukizingatia tulikuwa pungufu.


“Katika mchezo wetu huu, Yanga nimeona ilikuwa na mchezaji mmoja tu mzuri, yule aliyevaa jezi namba 27 (Msuva) kwani alikuwa akitusumbua sana kuliko wachezaji wengine wote wa Yanga,” alisema Kotei. 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic