February 28, 2017


Beki Method Mwanjale bado hajarejea katika hali nzuri licha ya kwamba alianza mazoezi taratibu lakini jana na leo ameshindwa kufanya kazi na wenzake.


Mwanjale aliumia goti katika mechi Simba ikiivaa Prisons na kulazimika kutolewa nje.

Kabla ya mechi dhidi ya Yanga, alionyesha matumaini lakini inaonekana bado hajawa vizuri.


“Tumefanya mazoezi siku mbikli sasa bila ya Mwanjale. Hatujajua kama anaendeleaje lakini inaonekana ametakiwa kupumzika,” kilieleza chanzo.


Simba iliifunga Yanga kwa mabao 2-1 bila ya Mwanjale na baada ya hapo, wachezaji wake walipumzika Jumapili kabla ya kuanza mazoezi jana na wameendelea leo lakini Mwanjale, hakupatikana siku zote mbili.
2 COMMENTS:

  1. Hivi hamna habari zingine za Michezo zaidi ya hizi za Simba na Yanga.
    Kila mkiweka habari ni ya Simba au yanga

    ReplyDelete
  2. Hivi hamna habari zingine za Michezo zaidi ya hizi za Simba na Yanga.
    Kila mkiweka habari ni ya Simba au yanga

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV