Pamoja na kutua nchini kujiunga na Simba, Juuko Murshind ameshindwa kufanya mazoezi na wenzake leo.
Juuko alikuwa kwao Uganda alipokwenda kuitumikia timu yake ya taifa, The Cranes na akaendelea kubaki Uganda akijiandaa kwenda Serbia ambako amepata timu.
Lakini uongozi wa Simba umefanya juhudi kubwa kuhakikisha anarejea na kujiunga na wenzake kwa ajili ya mechi inayofuata dhidi ya Mbeya City, Jumamosi, pia mechi nyingine zilizobaki.
Hata hivyo, Juuko hakutokea mazoezini wakati Simba ilipojifua leo asubuhi na taarifa zinaeleza, ataanza mazoezi na wenzake, kesho.
“Kweli leo hakuanza mazoezi, atafanya pamoja na wengine kesho,” kilieleza chanzo.
0 COMMENTS:
Post a Comment