February 7, 2017

Kikosi cha Simba, kimeendelea na mazoezi yake kujiandaa na mechi yao dhidi ya Prisons ya Mbeya, Jumamosi.


SImba imefanya mazoezi chini ya Kocha Joseph Omog ambaye ameonyesha kubadilika kwa kuifanya timu yake icheze kwa kushambulia zaidi.

Mazoezi ya Simba yamefanyika kwenye Uwanja wa Polisi Kilwa Road jijini Dar.

Katika mechi iliyopita, Simba iliitwanga Majimaji kwao Songea kwa mabao 3-0.Kabla Simba ilikuwa ikishinda kwa tofauti ya bao moja huku kikosi kikionyesha kujilinda zaidi. Katika mechi dhidi ya Majimaji, ilikuwa ikipeleka mashambulizi mengi zaidi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV