February 7, 2017


MAZOEZI YA YANGA KWENYE UWANJA WA UHURU, LEO


Yanga watapumzika wikiendi hii na suala la Ligi Kuu Bara. Lakini watakuwa na kibarua cha Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Ngaya ya Comoro.

Leo, kikosi hicho chini ya Kocha, George Lwandamina kimeendelea na mazoezi kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Yanga wameendelea kujifua kabla ya safari yao inayotarajiwa kuwa keshokutwa kwenda Comoro kuanza kampeni ya Ligi ya Mabingwa, msimu huu.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV