Simba wanaonekana kutotaka mchezo na mechi ya Jumamosi baada ya viongozi wake kwa asilimia 80 kuhamia Zanzibar.
Simba imeweka kambi Zanzibar kujiandaa na mechi yao ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Yanga, kesho Jumamosi.
Viongozi wengi wa kamati ya utendaji ya Simba wakiongozwa na Muslah Al Rawah wamekuwa Zanzibar kwa zaidi ya siku tatu sasa.
Wengi wao wako katika kundi la Friends of Simba na wameongozana na Rais wa Simba, Evans Aveva ambaye pia ni mmoja wa waanzilishi wa kundi hilo wakiwa wanataka kuona kila kitu kinakwenda sawa.
Wengine ni pamoja na Mohammed Kigoma pia Jamhuri Kihwelo ambaye hivi karibuni amekuwa akitumiwa kuwasaidia wachezaji kuinua morali.
Pamoja na kuzungumza na wachezaji kwa lengo la kuinua morali, wamekuwa wakizunguka kuhakikisha kila kitu kinakwenda sawa.
Taarifa zinaeleza, wanaweza kurejea Dar es Salaam leo na kikosi cha Simba pia kitafuatia.
0 COMMENTS:
Post a Comment