February 24, 2017

Taarifa za mwamuzi Mathew Akrama wa Mwanza kupewa dhamana ya kuamua mechi ya watani Simba dhidi ya Yanga, kesho ndiyo zimechukua nafasi zaidi.

Akrama hii haitakuwa mechi yake ya kwanza kuamua mechi hiyo na wachezaji wa pande zote mbili wanapaswa kuwa makini sana.

Simon Msuva wa Yanga anamkumbuka kwa kuwa aliwahi kumlamba kadi nyekundu.

Ni mtu anayefuata sheria 17 zaidi kuliko kuangalia suala na kupoza mambo.

Hivyo kama mchezaji atapata kadi ya njano, anapaswa kuwa makini maradufu zaidi.

Waamuzi wa akiba wanatarajiwakuwa wafuatao.
Line 1: Mohamed Mkono-Tanga

Line2: Hassan Zani -Arusha.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV