February 15, 2017Washindi watatu wa mbio za baiskeli waliopatikana katika Tamasha la Majimaji Selebuka, leo Jumatano wameagwa jijini Dar es Salaam tayari kwa safari ya kwenda Afrika Kusini kushiriki mashindano ya Dis-Chem Ride for Sight 2017.

Washindi hao ambao ni Salum Miraji, Allen Nyanginywa na Ipyana Mbogela, keshokutwa Ijumaa wataondoka nchini kwenda Afrika Kusini tayari kwa mashindano hayo yatakayofanyika Februari 19, mwaka huu katika Jiji la Johanesburg.


Akizungumza na waandishi wa habari, Mwandaaji Mkuu wa Majimaji Selebuka, Reinafrida Rwezaura, alisema: “Katika Tamasha la Majimaji Selebuka lililofanyika Juni 4, mwaka jana, kwa upande wa mbio za baiskeli kutoka Mbinga mpaka Songea, hawa ndiyo walikuwa washindi wetu.

“Hivyo baada ya kutoa ahadi ya kwamba tutawapelekea Afrika Kusini kushindana na wenzao, leo hii tunatimiza ahadi hiyo kwa kuwakabidhi tiketi tayari kwa safari yao ya siku ya Ijumaa.”

Katika hatua nyingine, Rwezaura, alisema katika tamasha la mwaka huu ambalo ni la msimu wa tatu, litafanyika Julai 23 mpaka 30, huku washindi watatu wa mbio za baiskeli nao watapata fursa kama hiyo ya kushiriki mashindano ya Afrika mwakani.Mambo yatakayofanyika katika msimu huu wa tatu ni pamoja na riadha mbio ndefu na fupi, mbio za baiskeli, midahalo katika shule za sekondari, mashindano ya ngoma za asili, maonesho ya biashara, utalii wa ndani, Majimaji Selebuka Mtu Kwao Forum na Majimaji Selebuka Mkabesa Platform.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV