February 7, 2017

Hatimaye wale watuhumiwa wa madawa ya kulevya ambao pia ni wasanii wa filamu na muziki pamoja na wafanyabiashara nchini wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kupewa dhamana Iliyoambatana na Masharti Matatu.
Khalid Mohammed T.I.D akiwa chini ya ulinzi


 Waliopanda kizimbani leo muda mfupi uliopita  ni Johan (muongozaji), Babuu, Dogo Hamidu, TID, Recho (wanamuziki), Tunda (muigizaji), Rajabu ambaye ni kaka yake Dogo Hamidu na Dj Rommy Jones.

Akisoma masharti hayo, Hakimu wa Mahakama ya Kisutu, Huruma Shaidi alisema kwamba watuhumiwa hao watatakiwa kufanya vitu vitatu mara tu watakapotoka mahakamani hapo.Kila mmoja alitakiwa kuweka bondi ya shilingi milioni kumi, kuripoti katika Kituo Kikuu cha Polisi, Dar mara mbili kwa mwezi kwa mwaka mzima huku pia wakitakiwa kuwa chini ya uangalizi wa mahakama kwa miaka mitatu mfululizo.

Kwa upande wa serikali katika kesi hiyo ilisimamiwa na Wakili Nassoro Katuga huku upande wa utetesi ukiwakilishwa na Wakili Albert Sando.

Kutokana na watuhumiwa kuingizwa kwa makundi mahakamani hapo, ni hao wachache ndiyo walioingia ila bado wengine wanatarajiwa kuingizwa dakika chache zijazo.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV