Timu gani itasonga mbele kwa kuingia hatua ya Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho Azam (Azam Sports Sports Federation Cup) kati ya Young Africans na Kiluvya United?
Majibu ya swali hilo yatakatikana kesho Machi 7, 2017 baada ya mchezo kati ya timu hizo utakaofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Utakuwa ni mchezo wa kukamilisha raundi ya sita ambayo ilikutanisha timu 16 Bora na inayofanya vema huingia hatua Nane Bora au Robo Fainali.
Mshindi kati ya timu hizo, itaungana na timu nyingine saba zilizotangulia kucheza Robo Fainali ambazo ni Simba na Azam FC za Dar es Salaam, Mbao FC ya Mwanza, Tanzania Prisons ya Mbeya, Madini ya Arusha, Kagera Sugar ya Bukoba na Ndanda FC ya Mtwara.
Bingwa wa michuano hiyo kwa mujibu wa kanuni, atazawadiwa Tsh. 50 milioni. Bingwa wa michuano hiyo, ndiye atakayeiwakilisha nchi kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika ya Total wakati Bingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara ndiye ataiwakilisha nchi kwenye michuano ya Total Ligi ya Mabingwa Afrika.
0 COMMENTS:
Post a Comment