SIMBA SPORTS CLUB
Dar es salaam, Tanzania
6/3/2017
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Vinara wa ligi kuu Tanzania Bara, Klabu ya Simba imekubali mwaliko wa Chama cha Soka mkoani Dodoma (DOREFA) Kwa ajili ya kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya Polisi ya mjini humo siku ya Jumamosi hii tarehe 11-3-2017.
Kwa kuwa klabu yetu haitakuwa na mchezo wa ligi kuu wikiendi ijayo, tunaamini washabiki wetu wa Dodoma na mikoa ya jirani watapata fursa adhimu ya kuiona ya timu yao. Pia tunatarajia kuutumia mchezo huo Kama maandalizi ya mechi yetu ya Kombe la Shirikisho hatua ya Robo fainali itakaochezwa machi 18.
Tunaamini pia buradani hiyo MUBASHARA, wataipata pia watumishi wa umma ambao wameshaanza kuhamia Makao makuu ya nchi kutekeleza agizo la Rais wa Jamhuri Dr John Pombe Magufuli
Imetolewa na
HAJI S MANARA
MKUU WA HABARI NA MAWASILIANO SIMBA SC.
SIMBA NGUVU MOJA
0 COMMENTS:
Post a Comment