March 16, 2017
Ahmad Ahmad ameuangisha mbuyu kwa kushinda Urais wa Shirikisho la Soka Afrika (Caf).

Ahmed raia wa Madagascar amemshinda Rais wa zaidi ya miaka 15 katika shirikisho hilo, Issa Hayatou raia wa Cameroon.


Mkutano Mkuu wa Caf ambao unaendelea sasa Ahmed amepata kura 34 huku Hayatou akipata 20 tu. 

HAYATOU (KATIKATI) AKIWA NA RAIS WA ZAMANI WA TFF, LEODEGER TENGA (KULIA) NA JAMAL MALINZI AMBAYE NI RAIS WA SASA WA TFF.

Hayatou amekuwa kiongozi wa Caf tokea mwaka 1988, maana yake amekuwa kiongozi wa shirikisho hilo kwa miaka 29.

Lakini Hayatou aliyezaliwa Agosti 9, 1945 alionekana kuwachosha wengi wakitaka mabadiliko.


Katika uchaguzi wa leo, ilionekana hakuwa na nguvu lakini bado alionekana ni mwenye nguvu ya kuitaka nafasi hiyo tena.

1 COMMENTS:

  1. Afadhali kaondoka maana ilikuwa too much

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV