March 16, 2017




Ile kesi inayomkabili Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji ya matumizi ya dawa za kulevya aina ya Heroine, imeshindiindikana kusikilizwa kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kupigwa kalenda hadi Aprili 18, mwaka huu.

Mtuhumiwa, Manji alishindwa kutokea kutokana na kusumbuliwa na maradhi ya moyo ambapo amelazwa katika Hospitali ya Aga Khan jijini Dar es Salaam.

Tuhuma zinazomkabili Manji ni kutumia madawa hayo kinyume na Sheria ya mwaka 2015 ya kuzuia na kupambana na madawa ya kulevya kifungu cha 17 (1) namba 5 ambapo inadaiwa Manji alitumia dawa hizo Februari 6 na 9, mwaka huu. 

Mashabiki mbalimbali wa soka walijitokeza mahakamani hapo kuifuatilia kesi hiyo.

Kesi hiyo ambayo inasikilizwa na Hakimu Mkazi Mfawidhi, Cyprian Mkeha huku upande wa Jamhuri ukiwakilishwa na Wakili Osward Tibaloyekomya huku upande wa Manji ukiongozwa na Wakili Alex Mgongolwa.

Kesi hiyo ilipangwa kusikilizwa jana Alhamisi lakini ilishindikana baada ya pande zote mbili kushindwa kutokea mahakamni hapo.


Manji yupo nje kwa dhamana ya milioni 10 aliyowekewa na Katibu wa Yanga, Charles Mkwasa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic