March 18, 2017


Na Mwandishi Wetu, Arusha
Baada ya kuonekana hayuko vizuri kifiziki aliporejea na kujiunga na Simba akitokea Uarabuni, mshambuliaji Frederic Blagnon ameendelea kujifua na wenzake.

Blagnon ameanza kuonekana kurejea hapa mjini Arusha ambako Simba imeweka kambi ikisubiri kuivaa Madini FC katika mechi ya Kombe la Shirikisho, kesho.


Katika mazoezi ya Arusha, Blagnon anaonekana kuanza kurejea vizuri kutokana na anavyokimbia bila kuchoka, usaidizi wake katika ukabaji, upigaji mashuti na pasi za mabao.

Kurejea kwake na kama akirejea katika hali nzuri, Blagnon atarejea katika ushindani wa namba dhidi ya Laudit Mavugo ambaye sasa yuko vizuri.

Kama atarejea asilimia mia, maana yake itaongeza ushindani na kuifanya Simba kuzidi kuwa na uhakika zaidi katika ushambulizi.

Kabla, Blagnon na Mavugo walionekana kudorora kwa muda mrefu na kushindwa kuisaidia Simba.

Lakini Blagnon akipelekwa Uarabuni kwa mkopo, Mavuko aliamka na kuanza kufanya vema.0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV