March 18, 2017
Kocha Mkuu wa Simba, Joseph Omog ameonyesha kuhusiana na suala la timu ya Madini FC wanayoivaa katika Kombe la Shirikisho, kesho.

Simba itashuka dimbani Sheikh Amri Abeid jijini Arusha kuivaa timu hiyo.

Omog amesema kwanza hawataidharau Madini FC, lakini kutoijua inaweza kuongeza ugumu kwao.

“Lazima wachezaji wajitume, lazima wawe makini na lazima tupambane.

“Hatuijui Madini, hata kama sisi ni bora lakini haiwezi kuwa uhakika tumeshinda. Lazima tucheze na kushinda,” alisema Omog.


Simba wamefanya mazoezi yao ya mwisho leo kabla ya kesho kupambana na Madini FC ambao wametamba, wako tayari kuituliza Simba.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV